Wahifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wametoa wasilisho la fursa za Uwekezaji zilizopo katika sekta ya Misitu, Nyuki na Utalii Ikolojia katika Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania katika mataifa ya nje (AMBASSADORS RETREAT, 2024) katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani.

Sambamba na hilo wahifadhi hao waliwapatia vipeperushi vyenye maelezo zaidi kwaajili ya kuweka kwenye balozi zao huku wakielezwa pia juu ya uwepo wa Mkutano wa 50 wa Apimondia ambao Tanzania ni mwenyeji kwa mwaka 2027 na kuwaomba kuunganisha nguvu katika kufanikisha Mkutano huo.