Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza Wa Tanzania kwenye Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sherehe hizo zimefanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.