Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole kutokana na kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe.Dkt.Hassan Sheikh Mohamud.

Viongozi hao walikutana leo tarehe 28 Aprili 2024 Ikulu , Migombani.

Mzee Mwinyi alifariki dunia tarehe 29 Februari, 2024 Dar es Salaam na kuzikwa tarehe 02 Machi 2024 kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Rais Dk.Mwinyi amemshukuru Rais Dkt.Mohamud kwa salamu za mkono wa pole na kuja kuwafariji.