Rais Samia Suluhu Hassan amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Shirikisho la Maendeleo la Kimataifa (IDA) umeleta maendeleo.

Akihutubia katika Mkutano wa Shirikisho la Maendeleo la Kimataifa (IDA) jijini Nairobi, Rais amesema  pamoja na miradi mingine, kwa ushirikiano na IDA nchi imeweza pia;-

  • Kuboresha eneo la afya ya mama na mtoto tukiwa na moja ya mifumo bora zaidi kwa ukanda wa Afrika,
  • Kuimarisha usambazaji umeme vijijini, eneo ambalo pia Tanzania ni moja ya nchi bora zaidi kwenye ukanda huu wa bara letu.
  •  Kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama, na
  • Kuanza kwa miradi mikubwa ya kudhibiti mafuriko hasa katika Jiji la Dar es Salaam ikiwemo mpango wa uboreshaji wa Bonde la Mto Msimbazi ili kudhibiti mafuriko ya mara kwa mara (Msimbazi Basin Development Project).

Katika hotuba yake,amesisitiza kuwa na sera bora za kifedha toka mashirika ya kimataifa kwa bara la Africa, zenye masharti na gharama nafuu, zinazotazama kuongeza uwekezaji katika kukuza rasilimali watu na teknolojia na kujikita zaidi katika kukuza uwezo wa kuongeza idadi ya mipango inayotekelezwa kati yake na nchi washiriki.