Nishati Safi ya Kupikia ni nini?

Nishati safi ya kupikia ni dhana inayotumika kuelezea na kubainisha vyanzo vya nishati na teknolojia fanisi ambapo kwa pamoja hutoa moshi wenye kiwango kidogo cha sumu pale zinapotumika kwa usahihi. Vilevile, nishati safi ya kupikia inatambulika kuwa salama, nafuu, endelevu na inayopatikana kwa urahisi. Dhana hii ina lengo la kupunguza athari za kimazingira na kiafya kwa watumiaji, pia ni nyenzo muhimu katika kutekeleza maazimio mbalimbali ya kitaifa na kimataifa katika kupambana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Mpango wa nishati safi kama utafika kijiji cha Kanga wilayani Songwe utawapunguzia adha wanawake ambao hivi sasa  bado wanafuata kuni milimani . Picha na LBM

Hali Ilivyo Sasa – Nishati & Teknolojia

  • Vinyesi vya wanyama
  • Kuni
  • Mkaa
  • Mafuta ya Taa
  • Mkaa Mbadala
  • Bayoethano
  • LPG
  • Gesi Asilia
  • Bayogesi
  • Umeme
  • Majiko Banifu
  • Majiko ya Nishati ya Jua

Idadi ya watanzania wanaotumia nishati safi ya kupikia ni asilimia 6.9 tu kwa mwaka 2021. Kiwango hiki ni chini ya kiwango cha wastani wa dunia cha asilimia 71 kwa mwaka huo.

Athari za Matumizi ya Nishati zisizo Safi za Kupikia ni zipi?

Athari za Kimazingira

Mabadiliko ya tabianchi ikiwemo kuongezeka kwa joto, mvua zisizokua na mpangilio, mafuriko, nk; • Kuongezeka kwa ukame (kiasi cha hekta 469,420 za misitu hupotea kwa mwaka kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo upataji wa kuni na mkaa.); na • Uharibifu wa mifumo ya kiikolojia ikiwemo kupungua kwa viumbe waliohatarini kupotea.

Athari za Kiafya

Vifo takribani 33,000 kwa mwaka; • Magonjwa sugu kama kikohozi, homa ya mapafu, kifua kikuu na saratani ya mapafu; • Kuharibika kwa ujauzito; • Kujifungua kabla ya wakati au kujifungua watoto wenye matatizo ya kiafya; • Magonjwa ya macho; • Kuathiriwa kwa uti wa mgongo, kichwa na miguu kutokana na ubebaji wa mizigo mikubwa ya kuni migongoni au vichwani; na • Kuelemewa kwa mifumo ya afya.

Athari za Kijamii

Ukatili wa kijinsia; • Kuhusishwa na imani za kishirikina; • Hatari ya kudhuriwa na wanyamapori; • Kukosa muda wa kuzalisha kipato; • Kukosa fursa za kushiriki shughuli za kijamii na kisiasa; na • Watoto kukosa muda wa kutosha masomoni.

Mkakati wa Taifa ya Matumizi ya Nishati

Safi ya Kupikia unahusu nini?

• Mkakati wa Taifa ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa Mwaka 2024 – 2034 umezinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 8, jijini Dar es salaaan na unatoa mwelekeo wa nchi wa kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia. Mkakati huu unatokana na hitaji la kuwa na mpango jumuishi wa kitaifa katika kupambana na ongezeko la uharibifu wa mazingira pamoja na athari za kiafya, kiuchumi na kijamii zinazotokana na matumizi ya nishati zisizo safi za kupikia.

Maandalizi ya Mkakati huu ni maelekezo mahsusi ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyotoa katika Mjadala wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia 2022 tarehe 01 Novemba, 2022.

• Lengo kuu la Mkakati ni kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Tamko la Mkakati

• Kila Mtanzania atumie nishati safi ya kupikia ili kulinda afya, mazingira na kuboresha maisha. Dhima • Kuhakikisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia iliyo nafuu, endelevu, salama na rahisi kutumika. Lengo Kuu • Kuhakikisha asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2033

Fursa zilizopo katika Nishati Safi ya Kupikia

Fursa za ajira na biashara zinazopatikana katika mnyororo wa thamani wa nishati safi ya kupikia:

 • Upatikanaji wa malighafi au vifaa (supply of raw materials or equipments) Mashamba, mabaki ya mimea, taka (majumbani,viwandani,taasisi), vinyesi, vifaa katika ujenzi wa miundombinu/mifumo ya nishati safi ya kupikia

• Uzalishaji (Production) Uzalishaji wa nishati safi, vifaa au majiko ya kupikia • Usambazaji (Distribution) Wakala wa usambazaji mfano: STAMICO

• Usafirishaji (Transportation) • Uhifadhi (Storage) • Ubunifu na uvumbuzi Katika nishati, teknolojia (mfano smart meters) na mifumo ya kibiashara (mfano PAY-AS-YOU-GO) • Ushiriki wa Wazawa Ajira katika utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia • Kipato kupitia utunzaji wa Mazingira (Biashara ya kaboni) • Mifuko na programu za kitaifa na kimataifa

Wanawake na Vijana wananufaika vipi na fursa hizo

• Kushiriki katika semina mbalimbali ili kupata elimu na mafunzo na kufahamu fursa zilizopo • Kujiendeleza katika fani mbalimbali na kuzifanyia kazi • Kutumia vikoba vyetu kuanzisha miradi midogo midogo ya utengenezaji wa majiko au mkaa mbadala • Fahamu mahitaji ya soko lako, fanya utafiti kujua nini kinauzika • Kuongeza ubunifu katika biashara (kukopesha, kuuza bidhaa kwa kiwango kidogo kidogo, mteja kulipia kidogo kidogo n.k) • Kuchangamkia fursa za mikopo na ruzuku kutoka kwa wadau mbalimbali UMEJIANDAA • Kuchangamkia fursa za uwakala

Serikali inawasaidiaje Wanawake na Vijana

• Kuandaa programu za utoaji elimu kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na fursa zilizopo kwa wanawake na vijana • Kutenga bajeti inayowezesha ushiriki wa wanawake na vijana katika miradi ya nishati safi za kupikia (Mfuko wa Nishati Safi ya Kupikia) – mikopo yenye riba nafuu, tuzo, ruzuku • Kutoa mafunzo ya uongozi kwa wanawake wasimamizi wa masuala ya nishati safi ya kupikia katika kila Halmashauri • Kuweka Sera zinazoweka mazingira wezeshi ya ushiriki wa wanawake na vijana

Kuhakikisha Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi vyote nchini vimejumuisha nishati safi ya kupikia katika mitaala yao • Kutoa mafunzo kwa wajasiriamali kuhusu nishati safi za kupikia katika kila Halmashauri • Kuwekeza katika tafiti mbalimbali ili rasilimali za ndani zitumike kutengeneza nishati, majiko na vifaa vya kupikia • Kutoa elimu ya kifedha kwa wadau wa nishati safi ya kupikia (kudunduliza/kufungua account, kuandika maombi ya ufadhili wa miradi n.k).