Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Mei 3, 2024  amekutana  na Mwenyekiti  wa Kamati Tendaji  ya Taasisi ya Huduma za Aga Khan, Mwana wa Mfalme Bi. Zahra Aga Khan na ujumbe wake, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
Mheshimiwa Waziri Mkuu amemwambia Kiongozi huyo kuwa Serikali inatambua jitihada kubwa zinazofanywa na Taasisi hiyo hasa katika sekta ya Afya na Elimu na amemuahidi kuwa serikali itaendelea kuunga mkono juhudi  za uwekezaji zinazofanywa na Taasisi ya hiyo.
Pichani, Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na  Mwana wa Mfalme, Zahra Aga Khan  (kulia kwake) pamoja na jumble wake.Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Naibu Waziri wa Afya, Det. Godwin Mollel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)